Mheshimiwa mkuu wa wilaya ya Tunduru adv. Julius S.Mtatiro leo mei 9,2023 ametembelea katika eneo linalotarajiwa kujenga shule mpya ya mkondo mmoja katika kata ya Tinginya kijiji cha Tinginya ambao ni mradi wa upatikanaji fursa sawa za ujifunzaji kwa elimu ya awali na msingi (BOOST)
Ambapo halmashauri ya wilaya ya Tunduru imepokea takribani shilingi 331,600,000.00/= kwa ajili ya mradi huo wa kujenga jengo la utawala (01),madarasa(09) (madarasa(2) ya awali na msingi(07)) ,matundu ya vyoo (10) na kichomea taka(01)
Mh.mkuu wa wilaya alishiriki na wananchi wa Tinginya katika uzinduzi wa ujenzi wa shule hiyo mpya kwa kufanya kazi pamoja nao na kupata fursa ya kuzungumza na wananchi wa Tinginya.
Aliagiza , vijana wote wa jeshi la akiba kijiji cha tinginya kukabidhiwa ajira ya ufyatuaji wa matofali ya mradi huo pia kuwaomba kujitolea katika ulinzi wa eneo la mradi, na vijana wengine kupewa ajira zitakazojitokeza kutokana na mradi huo .
Aidha mkuu wa wilaya ameitaka serikali ya kijiji iunde Kamati inayohusisha wananchi ya vifaa ambayo itakuwa inafuatili kwa ukaribu matumizi ya vifaa vyote vya ujenzi wa mradi huo, amesisitiza pia uaminifu wa kamati zote za manunuzi ,utunzaji na usimamizi wa mradi
Mwisho aliwataka Wananchi wa Tinginya kuulinda mradi kwa hali ya uzalendo ili uweze kukamilika kwa wakati na kwa usahihi mkubwa.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.