Mheshimiwa mkuu wa wilaya ya Tunduru adv. Julius S. Mtatiro , amezungumza na wananchi leo mei 8, 2023 katika kata ya Ligoma kijiji cha ligoma kuhusu mradi wa ujenzi wa shule mpya yenye mikondo miwili (2) ambayo imewezesha na mradi wa upatikanaji wa fursa sawa katika ujifunzaji bora wa elimu ya awali na msingi Tanzania bara,(BOOST).
Katika mazungumzo na wananchi hao mheshimiwa mkuu wa wilaya amewaagiza watendaji wa mradi huo kuendeleza uzalendo katika miradi ambayo inaletwa na serikali ili kuifanya iwe bora na kukamilika kwa wakati na kwa usahihi.
Ameitaka kamati ya mradi huo kusimamia kwa uadilifu na kuweka taarifa za manunuzi ,utunzaji na matumizi ya vifaa vya kutimiza ujenzii huo wa shule hiyo.
Pia amemtaka muhandisi wa wilaya Ramadhani R. Magaila ambaye ni msimamzi wa ujenzi wa mradi wa shule hiyo kuandaa ripoti ya taarifa inayohusu matumizi ya vifaa vyote vya ujenzi vitakavyokuwa vinatumika katika mradi huo .
Aidha mkuu wa wilaya amewataka wananchi kuonesha ushirikiano katika kuboresha na uthibiti wa ukamilishaji wa miradi hiyo kwa kufuatilia na kutoa taarifa mapema pale wanapohisi kuna utendaji usio sahihi katika mradi huo.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.