Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mhe. Wakili Julius S. Mtatiro amewasisitiza viongozi na watendaji wote kuwa waadilifu na kufuata miiko na maadili ya kazi wawapo katika kutekeleza majukumu yao. Aliyasema hayo akiwa katika mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji cha Ligunga kilichopo wilayani Tunduru.
Pichani:Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya.
Mhe. Wakili Mtatiro amempumzisha kazi Mtendaji kata wa kata ya Ligunga, Bi. Mercy Ajabu kwa kushindwa kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kazi kikamilifu. Aliagiza kwamba Mtendaji kata huyo apangiwe kituo kingine huku akiagiza kijiji hicho kipelekewe Mtendaji mwingine.
Aidha, Mhe. Wakili Mtatiro aliagiza Meneja wa Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA), Mhandisi. Maua Mgala, kufika haraka siku ya jumanne ya tarehe 30.01.2024 katika kijiji cha Ligunga na kufanya tathmini upya ya maji kuondoa changamoto ya uhaba wa maji inayowakumba wakazi wa kijiji hicho.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.