Mkuu wa wilaya ya Tunduru Mheshimiwa, Wakili Julius S. Mtatiro alihudhuria baraza la madiwani la robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2023/2024,Novemba o1,2023 katika ukumbi wa klasta-Mlingoti , ambapo ameelekeza nakutoa maagizo yanayolenga kuimarisha maendeleo.
Katika maagizo yake, Mh. Wakili Mtatiro aliagiza Miradi yote ya maendeleo ikamilike kwa wakati, pamoja na kuwepo changamoto kadhaa, aagiza wataalamu na wasimamizi kuzifanyia kazi haraka iwezekanavyo ili ikamilike na wananchi waanze kupata huduma.
Kuhusu kilimo, Mh. Wakili Mtatiro alitoa maelezo juu ya mbolea. Alisema, kutakuwepo na mfumo utakaomwezesha mkulima kupokea mbolea bila kupoteza muda na kutumia gharama kubwa za usafiri. Maelekezo haya yataleta tumaini kwa wakulima walioko vijiji vya mbali.
“Utaratibu wa viuatilifu umekamilika, tumekutana na makampuni tumepanga mpango kazi, nimeruhusu kampuni hizo kukutana na ushirika pamoja na vyama vya ushirika” Alisema. “Mbolea itakua kwenye ghala, na wananchi watakuwa wakikusanya fedha zao za mbolea kwenye AMCOS, kampuni hizi zitakuwa zikichukua mbolea na kuipeleka kwa mkulima mahali alipo, gharama za kupandisha na kushusha zitakua juu ya kampuni, lengo ni kuondoa gharama kwa mwananchi kusafiri toka vijiji vya mbali kufuata mbolea mjini”.
Akizungumza katika Baraza hilo, aliagiza pia ufugaji holela kukomeshwa kwani ardhi ya Wilayani Tunduru ni kwa ajili ya kilimo, alisema, ufugaji holela unasababisha uharibifu wa mazingira na kuzorotesha uzalishaji wa mazao, wafugaji waende maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli hiyo.
Maagizo hayo ya Mkuu wa Wilaya yanalenga kuboresha hali ya maisha,Ukamilishaji wa miradi ya maendeleo utaleta fursa na utasaidia katika upatikanaji wa huduma bora, Kukomesha ufugaji holela kutasaidia kulinda ardhi ya wananchi wa Tunduru. Pia, upatikanaji wa mbolea kwa urahisi hasa kwa wananchi waishio vijijini utasaidia kuongeza tija katika kilimo.
Imeandaliwa na Orpa Kijanda, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.