Mh.Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Bw. Julius Mtatiro amekamata zaidi ya tani kumi za korosho Chafu ambazo zimeingia Wilaya ya Tunduru kutoka Wilaya na Mikoa ya Jirani ambapo korosho hizo zingefanikiwa kuuzwa zingeongeza kushuka kwa ubora wa korosho za Tunduru.
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Tunduru amesema baadhi ya vyama vya msingi vya kukusanya mazao ya wakulima Wilaya ya Tunduru havina uzalendo ndivyo upokea korosho chafu zinazo toka kwenye wilaya na mikoa ya jirani na kuletwa Wilaya ya Tunduru kuuzwa na viongozi hao wa vyama vya msingi uzipokea korosho hizo kwa Maslai yao binafsi.
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru alikitaja Chama cha Msingi cha Mlingoti Mashariki ni moja kati ya chama cha msingi cha mfano kilicho pokea korosho chafu kutoka Wilaya na mikoa ya jirani kwajili ya maslai yao binafsi ya Viongozi hivyo alimtaka OCD awashikilie viongozi hao wa Chama cha msingi cha Mlingoti Mashariki adi pale upelelezi utakapo kamilika.
Aidha Mkuu wa wilaya ya Tunduru amekiagiza chama cha ushirika cha Mlingoti Magharibi kichukue nafasi ya Chama cha msingi mlingoti mashariki kitakusanya majuku yote ya kukusanya korosho ambazo zimebaki kwa msimu huu uliobaki pia Dc mtatiro ametoa onyo kali kwa Vyama vingine vya msingi kuwa msako unaendelea kila Amcosi.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.