Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Bw. Julius Mtatiro amekabidhi pikipiki kwa Maafisa kilimo wa Wilaya ya Tunduru uku akiwataka kuwa wawatumikie wakulima kwa uadilifu mkubwa kwani kabla ya kupata pikipiki hizo maafisa kilimo wengi walikuwa hawaendi kuwatembelea wakulima kwa kisingizio kuwa hawana usafiri.
Aidha Dc Mtatiro amewataka Maafisa kilimo hao kuwa hizo pikipiki sio za kufanyia starehe au mizunguko yao binafsi endapo ikibaina kuna afisa kilimo anatumia pikipiki hizokinyume na malengo ambayo yalitarajiwa hivyo hatua kali itachukuliwa zidi yake.
Dc aliendelea kusema pongezi nyingi zimuendee Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Samia Suluu Hassani kwa kuipatia Wilaya ya Tunduru Pikipiki 64 za Maafisa Kilimo uku matarajio ya serikali ni kuona uzalishaji unaongezeka mara mbili kuliko sasa.
Pia aliwataka maafisa kilimo hao wawatembelee wakulima na kuwapatia elimu ya kilimo bora na chenye tija endapo ikitokea kuna afisa kilimo ambae hatimizi majukuu yake ipasavyo basi hatua za kinidhamu zitachukuliwa zidi yake .
Kwa upande wake Kaimu mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Bw.Jonathani Haule alisema ameyapokea maagizo yote yaliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Tunduru na atayatekeleza kwa Vitendo.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.