Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Mhe. Denis Masanja ameongoza kikao cha tathmini na kupanga mikakati mipya ya kuimarisha uhifadhi na kupunguza migongano kati ya binadamu na wanyamapori, kilichofanyika kwa ushirikiano na Wakala wa Huduma za Wanyamapori Tanzania (TANAPA).
Kikao hicho kimejikita katika kutathmini utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Shirika kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2020/21. Ambapo mafanikio na changamoto za kiuhifadhi ziliainishwa ikiwa ni pamoja na uharibifu wa mazao na Mali za wananchi unaosababishwa na wanyamapori husisani katika vijiji vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa ya Nyerere pamoja na vile vilivyopo katika ushoroba wa Selous-Niasa
Miongoni mwa yaliyopendekezwa ni pamoja na:
1. Kutoa elimu endelevu kwa jamii kuhusu namna bora ya kuishi kwa amani na wanyamapori na kutatua migongano bila kutumia nguvu.
2. Kuwezesha mipango ya matumizi bora ya ardhi ili kuzuia uvamizi wa maeneo ya wanyama na binadamu.
3. Kuimarisha doria za pamoja (joint patrols) kati ya TANAPA, Halmashauri na vyombo vya ulinzi ili kudhibiti ujangili na uharibifu wa mazingira.
4. Kujenga vituo vya kudumu vya PAC katika vijiji vinavyoathirika zaidi.
5. Kuongeza vitendea kazi kama magari, ndege ndogo za doria, na helikopta kwa ajili ya kudhibiti wanyamapori waharibifu.
6. Kuendeleza ushirikiano na jamii kwa kuajiri na kutumia Vijana wa Gawio la Uhifadhi (VGS) ili wajisikie sehemu ya jitihada za uhifadhi.
Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Masanja alisisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano kati ya wananchi na taasisi za uhifadhi, akisema kuwa maendeleo endelevu hayawezi kupatikana bila uhifadhi imara wa mazingira.
Aliongeza kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha migongano kati ya binadamu na wanyamapori inapunguzwa au kuondolewa kabisa, huku jamii ikinufaika na rasilimali za uhifadhi.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.