Aliyasema hayo katika mkutano wa hadhara wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi uliofanyika katika kijiji cha Nasya mapema wiki alipofika kukagua eneo lililotengwa kwa ajili ya kujenga zahanati ya kijiji hicho.
Akisoma taarifa ya kijiji hicho afisa mtendaji wa kijiji hicho alisema ujenzi wa zahanati hiyo ulianza mwaka 2012 kwa kutenga eneo lenye ukubwa wa ekari nne, na kuanza kumwaga jamvi na jumla ya shilingi milioni 11 zilitolewa kupitia mfuko wa jimbo katika awamu mbili kwa mwaka 2012 na mwaka 2016.
Aliendelea kusema kuwa wananchi wameendelea kupata tabu ya kutembea umbali mrefu kufata huduma katika zahanati ya kijiji cha Tuwemacho na kituo cha afya Mtina, huku wakikumbana na changamoto kubwa hasa kipindi cha masika.
Akizungumza na wananchi mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Zuberi Homera alianza kwa kuwapongeza wananchi kushiki kikamilifu katika kuanzisha ujenzi wa zanahati hiyo, huku akitoa ahadi ya mifuko 100 ya saruji kwa ajili yakuendeleza ujenzi huo.
katika picha ni wanachi wa kijiji cha nasya Kata ya Tuwemacho Kijiji cha Nasya wakiwa katika mkutano wa Hadhara na Mkuu wa wilaya ya Tunduru Mh. Juma Zuberi Homera ulifanyika tarehe 16/03/2019
"mimi nitachangia mifuko mia moja ya saruji kwa ajili ya kuendeleza ujenzi na wananchi nawaagiza kukusanya mchanga kutoka mto Msenjewe, kila kitongoji mpangiane ratiba ya kwenda kuopoa mchanga mtoni"alisema mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera.
Sambamba na hayo Mkuu wa Wilaya aliutaka uongozi wa kijiji hicho kutunza eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya kwa kuzungushia uzio ili kuepkuka uvamizi unaofanywa na watu wasiokuwa na huruma wananchi hasa kinamama wanaosafiri umbali mrefu kufata huduma za afya.
Juma Homera alisema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Nasya kutaondoa changamoto ya huduma za afya kwa kinana na watoto kwa kusogeza huduma karibu na wananchi lakini pia kupunguza vifo vya mama na mtoto kutokana na kutembea umbali mrefu kupata huduma katika vijiji vya Mtina na Tuwemacho.
Kwa upande mwingine Afisa afya Ndg Ayubu Joseph Majumbawima aliwataka wanawake wajawazito wanapojigundua mara ni wajawaziti kuanza kliniki mara moja ili kupata dawa za kumkinga mtoto na malaria , vyandarua na kupima afya pamoja na wenza wao.
Diwani wa Kata ya Tuwemacho Mhe.Hadija Timamu akieleza changamoto za wananchi wa kijiji cha Nasya katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini tarehe 16/03/2019
Ayubu aliendelea kusema kuwa ili kutokeza malaria katika kijiji cha naysa ni vyema wananchi wakazingatia usafi wa mazingira kwa kuvyeka nyasi katika kijiji na maeneo yanayozunguka nyumba zao kwani hayo ndio masalia ya mbu wanaoeneza malaria.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.