DC Chacha atoa Tahadhari Kuhusu Mmomonyoko wa Ardhi Tarafa ya Matemanga
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Mheshimiwa Simon Kemori Chacha, ametoa tahadhari kwa wakazi wa Tarafa ya Matemanga, Kata ya Matemanga kufuatia mmomonyoko wa ardhi uliotokea katika eneo hilo tarehe 24 na 25 Aprili 2024.
Mhe. Chacha amewataka wakazi wa eneo lililoathiriwa kuondoka na kuepuka maeneo yaliyo karibu na eneo la tukio ili kuepusha hali ya hatari itakayoweza kutokea.
Aidha, Dc Chacha Ameongeza kuwa amewasiliana na mamlaka husika ili waweze kufika eneo la tukio kuchunguza chanzo cha mmomonyoko huo na kuchukua hatua za kudhibiti hali hiyo.
Mhe. Chacha amesema alipokea taarifa kuhusu tukio hilo na ameagiza uongozi wa eneo hilo kuchukua hatua za haraka kuwaondoa wakazi hao na kuhakikisha usalama wao. Serikali pia imetenga fedha kwa ajili ya kusaidia waathiriwa wa mmomonyoko huo
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema ni mara ya kwanza kutokea katika eneo hilo na hakuna ripoti ya vifo vilivyotokea, ingawa baadhi ya nyumba zilizokuwa karibu na eneo la tukio zimepata nyufa katika kuta na sakafu.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.