• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Tunduru District Council
Tunduru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maliasili na Utalii
      • Ushirika
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Mawasiliano Serikalini
      • Michezo,Utamaduni na Sanaa
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Biashara na Viwanda
    • Mining
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Huduma za Watumishi
    • Elimu
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
    • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha za Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Time Table
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Tarajali
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa wateja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

BILIONI 3.7 zaingia katika mzunguko Tunduru.

Imewekwa : August 31st, 2023

Wakulima wa Mbaazi Halmashauri ya wilaya ya Tunduru wameingiza katika mzunguko zaidi ya bilioni 3.7 kupitia zao la Mbaazi.

Mnada wa tatu wa uuzaji wa Mbaazi uliofanyika kijiji cha Angalia Kata ya Mtina,katika ofisi za Chama cha Ushirika cha Mshikamano ulikuwa na mafanikio makubwa. Jumla ya tani 1928 za Mbaazi ziliuzwa katika mnada huo, ambazo ni sawa na kilo milioni 1.9.

Idadi ya wanunuzi katika mnada huo ilikuwa 20, hata hivyo ni wanunuzi 6 tu ndio ambao walikaribia bei iliyotarajiwa na wakulima. bei ya juu ilikuwa shilingi 1,950 na kufanya bei wastani kuwa shilingi 1,946. Wakulima walikubali kuuza Mbaazi  kwa bei ya wastani ya shilingi 1,948. Hii inaonyesha kuwa uuzaji ulikuwa na ushindani mkubwa kati ya wanunuzi.

Aidha Mlajisi Msaidizi vyama vya Ushirika mkoa wa Ruvuma Bi. Peja muhoja amewasisitiza wakulima wa mazao yote ya biashara kuacha kuuza mazao yao kwa mtu kati (mlanguzi), na kuwataka kutumia mfumo wa Stakabadhi ghalani wenye manufaa makubwa kwa mkulima.

"Zao la Mbaazi limekuja na bei nzuri ,wakulima wakaongeze juhudi shambani, mashamba mapya na wayapande katika utaratibu wa kuzingatia kanuni bora za kilimo, vile vile fedha wanazozipata wakazitumie vyema kwa maendeleo yao Binafsiā€. Alisema.

Pia kwa upande wake mwenyekiti wa Chama kikuu cha Ushirika Tunduru Ndg. Mussa Manjaule amewasisitiza wakulima kuzidi kutanua na kuwekeza zaidi katika kilimo ,pia amewasisitiza wakulima kulima mazao mbalimbali mbadala ya chakula,kutokujikita kwenye zao la aina moja tu.

Zao la Mbaazi limepanda thamani katika soko ukilinganisha na kipindi cha nyuma, ambapo lilikua likionekana kama zao la chakula pekee,lakini kwa sasa limeingia katika mkakati wa kibiashara kwa kuuzwa zaidi ya shilingi 1,500. Bei hii inaweza kuwa chanzo cha kuridhika kwa wakulima na inaweza kuwachochea kuendelea kulima Mbaazi kwa wingi.

Imeandaliwa na Orpa Kijanda kaimu kitengo cha MawasilianoSerikalini Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru.


Matangazo

  • MKOPO WA HAZINA KWA WATUMISHI WA UMMA FUNGU 82N2 March 25, 2025
  • TANGAZO LA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA UTARATIBU WA KUJITOLEA October 01, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA December 12, 2024
  • ORODHA YA MAJINA YA WANAOTAKIWA KUSHIRIKI USAILI WA AJIRA YA MUDA YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KATIKA WILAYA YA TUNDURU January 12, 2025
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • KIKAO CHA ROBO YA KWANZA CHA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA LISHE KATA NA WILAYA CHAFANYIKA TUNDURU.

    November 18, 2025
  • KAMATI YA LISHE Tunduru Yajadili Mikakati Ya Kuimarisha Afua Za Lishe Katika Jamii.

    November 13, 2025
  • DC MASANJA AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA MRADI WA MAJI MSINJI, ATAKA UKAMILISHWE HARAKA

    October 24, 2025
  • DC MASANJA ATOA WITO WA AMANI KWENYE UCHAGUZI, AENDELEA KUPIGA VITA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI TUNDURU.

    October 23, 2025
  • Ona Zote

Video

RC RUVUMA AWAPA POLE WANANCHI AMBAO NI MAJERUHI WA MGOGORO BAINA YA WAFUGAJI NA WAKULIMA TUNDURU
Video Nyingine

viunganishi vya Haraka

  • MATOKEO YA MITIHANI
  • Mkataba wa huduma kwa Mteja
  • muongozo wa Tehama
  • Ijue Sheria ya Umiliki wa Ardhi ya Mwaka 1999
  • Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Tunduru

Tovuti linganifu

  • Tovuti Kuu ya Rais - IKULU
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Idara ya Habari Maelezo

wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Tunduru

    Anuani ya Posta: 275, TUNDURU

    Simu: + 255-025-2680004

    Simu ya Nununu:

    Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz

Anuani nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Kituo

Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.