Leo januari 19,2023 umefanyika mnada wa mwisho kwa upande wa zao la korosho kwa mikoa ya Ruvuma,Njombe na Mbeya ambapo mnada huo umefanyika katika wilaya ya Tunduru kama ni sehemu ya kufanyia minada hiyo ya korosho kwa mikoa tajwa hapo juu.
Katika mnada wa leo kulikua na idadi ya kilo 168,237 za korosho katika maghara yote yaliyokuwa yanatunza korosho ambapo daraja la kwanza (1) zilikua kilo 94,643 na daraja la pili (2) zilikua 73,594, wanunuzi watatu walipendekeza bei zao kwa ajili ya kununua korosho hizo zote zilizopo gharani, ambapo baada ya kufanyan uchakataji mnunuzi mmoja aliweza kununua korosho zote zilizopo gharani kwa bei, kama ifuatavyo:-
Kutokana na minada yote kumi iliyopita takribani kilo 15,099,235 ziliuzwa hadi kufikia mnada huo wa kumi (10) na kufanya kiasi cha shilingi bilioni 26.7 kuingia katika mzunguko wa mauzo ya korosho kutoka katika mikoa mitatu ambayo inalima korosho kwa nyanda za juu kusini yaani mkoa wa Ruvuma, Njombe na Mbeya kwa msimu wa korosho 2022/2023 .
Pia Wakulima watakiwa kufanya maandalizi mapema ya mashaamba yao kuanzia sasa ili kupata korosho bora kwa msimu ujao wa mauzo wa mwaka 2023/2024.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.