Serikali ya awamu ya sita imetoa bilioni 1.2 kuboresha miundombinu ya hospitali kongwe iliyoanzishwa mwaka 1930 wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma.
Mganga mfawidhi wa hospital ya wilaya ya Tunduru, Daktari Athumani Mkonoumo amesema wamepokea shilingi milioni 900 kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya hospitali hiyo ambayo inajenga maabara mpya, Jengo la wagonjwa wa nje (OPD) na chumba cha upasuaji.
Amesema Serikali pia imetoa shilingi milioni 300 kwa ajili ya ujenzi wa Jengo ya wagonjwa wa Dharura (EMD), na kwamba limekamilika na kuanza kutoa huduma za dharura tangu Juni mwaka huu.
Vilevile, hospitali imepokea vifaa vya matibabu katika jengo hilo la dharura (EMD), vifaa hivi ni pamoja na Mashine ya X-Ray, Utrasound, mashine za kusaidia kupumua pamoja mitungi ya gesi, ambapo hadi sasa wagonjwa zaidi ya 86 wamefanikiwa kupatiwa huduma zinazotolewa na EMD.
“Itatusaidia sana kutoa huduma bora na stahiki kwa sababu hatutokua na changamoto kubwa ya vifaa na miundombinu sahihi ya kutoa hizo huduma”. Alisema.
Ukarabati huu mkubwa wa hospitali utapunguza idadi kubwa ya wagonjwa kupewa rufaa ya kwenda kupata huduma nje ya wilaya.
Imeandaliwa na Orpa Kijanda, kaimu kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru.
21/08/2023.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.