Leo tarehe 17/06/2021 ulifanyika mnada wa 4 wilayani Tunduru. Jumla ya kilo zilizo kuwa zinauzwa leo ni 282,477 na jumla ya kampuni 4 walijitokeza kuomba kununua ufuta wa Tunduru ambao ni
1.EXPORT Trading Ltd kilo 282,477 kwa kilo 1 Tzs 1,935/
2. Yihai Kerry kilo 282,477 kwa kilo 1 Tzs 2,220/=
3. Afrisian Ginning Ltd kilo 282,477 kwa kilo 1 Tzs 2,318/=
4.Lenic Tanzania Ltd kilo 282,477 kwa kilo 1 Tzs 2,322/=
Wakulima waliridhia kumuuzia mnunuzi Lenic Tanzania Ltd kilo zote 282,477 kwa bei ya kilo 1 Tzs 2,322/= Sawa na Tzs 655,911,594/=.
Mnada wa leo ulifanyika Kata ya Marumba, kijiji cha marumba katika tarafa ya Nalasi.
Aidha Mwenyekiti wa Tamcu Ndugu Mussa Manjaule amewataka Wakulima kuongeza bidii ya kulima ufuta na kuacha kutegemea zao moja la korosho tu kama zao la kibiashara hivyo wakulima wa Tunduru waongeze bidii katika kuzalisha zao la ufuta ili likiyumba zao moja la kibiashara wanapata kwenye zao lingine la kibiashara.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.