Halmashauri ya wilaya ya Tunduru umefanyika mnada wa kwanza wa korosho tarehe 28/10/2021 mnada umefanyikia katika Tarafa ya Nakapanya kata ya Namakambale uku Kampuni ambazo zilijitokeza kutuma maombi ya kununua mzigo wa korosho zilikuwa 6 ambapo Kilo 1,745,804 za Korosho zipo sokoni kwa mnada huu wa kwanza wa korosho kampuni zilizo omba kununua mzigo ni kama zifuatavyo:-
1.Alfa Namata company ltd Kilo 200,000 kwa bei kg 1 Tzs 2100/=
2.Sibatanza company ltd Kilo 1,745,804 kwa bei kg 1 Tzs 2150/=
3.Eljai Commodities Company ltd kilo 500,000 kwa bei kg 1 Tzs 2109/=
4.Amj Buying and Transportation ltd kilo 450,000 kwa bei kg 1 Tzs 2109/=
5. PSL Company ltd kilo 1,745,804 kwa bei kg 1 Tzs 2010/=
6.Iscony commodities ltd 1,745,804 kwa bei kg 1 Tzs 2050/=
Wakulima walilidhia Kampuni ya Sibatanza inunue mzigo wote wa korosho kilo 1,745,804 uliopo sokoni kama kampuni ilivyo omba na kufanya Tzs 3,753,478,600/= kuingia kwenye mzunguko Wilayani Tunduru.
Aidha Mwenyekiti wa Chama kikuu cha ushirika (tamcu) Bw.Mussa Manjaule amewashauri wakulima waongeze bidii katika uzalishaji wa mazao ya kibiashara uku akiwaambia kuwa utaratibu wa ugawaji wa pembejeo msimu ujao utakuwa wa kulipia na sio bure hivyo wakulima wakae na kujua hilo.
Mh. Julius Mtatiro Mkuu wa Wilaya ya Tunduru ambae ni Mgeni mwalikwa katika mnada huo wa kwanza kwa msimu 2021-2022 amewataka Wakulima kuto tegemea zao moja la korosho kibiashara badala yake walime na mazao mengine ya kibiashara kama vile Soya na ufuta lengo ni kumfanya mkulima kuwa na fedha kwa kipindi chote cha mwaka.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.