Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru iliandaa hesabu zake kwa kipindi kinachoishia Juni 30, 2017 kwa kuzingatia viwango na vigezo vya ufungaji wa hesabu kwa taasisi za Umma (IPSAS) na taarifa hizo kukabidhiwa kwa Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tunduru imepata Hati safi (Unqualified Opinion). Jukumu la Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa fedha za Serikali ni kukagua fedha zote za Serikali Kwa mujibu wa Ibara ya 143 ya katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, 1977 (kama ilivyorejewa 2005) na kifungu cha 45 na 48(1) cha Sheria ya Fedha za Serikali za mitaa No 9 ya 1982 (kama ilivyorejewa 2000) pamoja na kifungu cha 10(1) cha Sheria ya Ukaguzi No 11 ya mwaka 2008.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Tunduru Ndg Chiza Cyprian Marando amesema kuwa pamoja na Tunduru kupata Hati Safi, kuna mambo ya msisitizo ambayo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa fedha za Serikali alisisitiza na kuitaka menejimenti kutoa majibu. Aidha Halmashauri imetoa majibu kwa hoja zote 68 za miaka iliyopita na mapendekezo ya hoja 24 kwa mwaka 2016/2017 ndani ya siku 21 kama sheria ya ukaguzi No 11 ya mwaka 2008 inavyoelekeza.
Mkutano wa Baraza la Madiwani umekamilika katika Ukumbi wa klasta ya Mlingoti huku Waheshimiwa madiwani wakiweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha Halmashauri haipati hoja mpya katika mwaka wa fedha 2017/2018, na zilizopo kuzipatia majibu kwa wakati.
Imetolewa na
Theresia Mallya
Afisa Habari Halmashauri.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.