Baraza la Madiwani la robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2023/2024 limefanyika Novemba 01,2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Klasta-Mlingoti, mkutano huo uliongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru, Mheshimiwa Hairu Mussa.Lengo kuu la mkutano huo lilikuwa ni kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo za Halmashauri kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2023/2024.
Mkutano huo ulianza kwa kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo za kata kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2023/2024. Taarifa hizo ziliwasilishwa na kamati za baraza la Madiwani ambazo ni kamati ya fedha,uongozi na Mipango, Kamati ya Uchumi,ujenzi na Mazingira, Kamati ya Huduma za jamii,Kamati ya Maadili pamoja na Kamati ya kudhibiti ukimwi.
Mhe. Hairu amewapongeza wataalamu na watendaji wote katika Halmashauri, na pia kuwaomba wasimamie kikamilifu ukusanyaji wa mapato pamoja na usimamizi wa miradi ya maendeleo ambayo inaendelea kutekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru.
“Elimu itolewe juu ya viuatilifu ili kuongeza tija kwenye sekta ya kilimo, kwani wanachi wengi Wilayani Tunduru wanategemea kilimo” alisema. “kazi kubwa ya Diwani ni kusimamia hali ya uchumi, niwaombe sana twende tukawashawishi wananchi kupeleka korosho zao ghalani, lakini pia tuhakikishe tunapata ushuru ambao utasaidia katika kujenga miundombinu Wilayani kwetu”
Waheshimiwa madiwani wameadhimia yafuatayo katika kuhakikisha kuwa Halmashauri inafikia malengo yake iliyojiwekea katika kuleta maendeleo kwa wananchi, maadhimio hayo yalikuwa ni kuhakikisha mtaalamu anaenda kukagua na kufuatilia ukusanyaji wa mapato, hasa mapato ya yatokanayo na mazao, taarifa ya wakulima wanaolima katika bonde la mto Masonya kuwasilishwa katika Baraza lijalo, Meneja wa TANESCO kuwasilisha michoro ya mradi wa umeme maeneo ya vijijini, Makorongo
Imeandaliwa na Orpa Kijanda, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.