Leo mei 13,2023 limefanyika baraza la madiwani la kawaida la robo ya pili katika wilaya ya Tunduru , la kujadili taarifa mbalimbali na mapato na matumizi katika wilaya ya Tunduru kwa kupitia taarifa za kamati zote, kamati ya fedha,kamati ya huduma za kijamii,kamati ya uchumi,ujenzi na mazingira pamoja na kamati ya uthibiti wa gonjwa la ukimwi.
Aidha mkutano huo wa Baraza uliudhuriwa na mheshimiwa mkuu wa wilaya ya Tunduru adv. Julius s. Mtatiro ambaye alitoa salamu za serikali kwa madiwani, mh. Mkuu wa wilaya aliwaomba madiwani kusimamia na kuhakikisha kufikia lengo la halmashauri la kufikia juu ya 80% ya mapato ya halmashauri ambayo kwa sasa yamefikia 74%.
Pia aliwaomba kuhakikisha na kuwasimamia maafisa ugani katika utendaji wao wa kazi katika maeneo yao ya kazi waliopangiwa, sambamba na ilo aliwasihi maafisa ugani kutotumia mali za serikali kinyume na matumizi yake yaliyokusudiwa kama vile pikipiki(boda boda)
Pia mkuu wa wilaya aliahidi kuzidi kutekeleza ahadi ya kuthibiti wanyama hatarishi hasa tembo, kwa kuongeza uwezo wa vifaa na miundombinu ya kuthibiti wanyama hao.
Utaratibu wa ugawaji viuatilifu msimu huu wa 2023/2024 utakuwa kupitia chama kikuu cha ushirika na vyama vyake vya msingi Tunduru ili kuwafikia wakulima kwa uhakika,aliyasema hayo mkuu wa wilaya ya Tunduru katika mkutano wa baraza la madiwani leo.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.