Jumuiya ya Wilaya ya Tunduru ilipokea taarifa za uhamisho wa Mkuu wa Wilaya, Mhe. Julius S. Mtatiro, ambaye amehamishiwa Wilaya ya Shinyanga. Na imempongeza kwa kuendelea kuaminiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Pichani ni Mhe. Julius S. Mtatiro
Wakati wa uongozi wake, Mhe. Mtatiro ameacha alama ya kudumu katika sekta ya elimu na kusimamia ajenda nyingine zote za maendeleo wilayani Tunduru. Mhe. Mtatiro alikuwa akithamini sana elimu na kuipa kipaumbele cha juu. Alikuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kila mtoto anayepata fursa ya kujiunga na elimu anapata elimu bora. Aliongoza kwa mfano kwa kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa elimu na kuwahimiza wazazi kuwapeleka watoto wao shule.
Sambamba na hayo, Mhe. Mtatiro Aliongoza juhudi za kuboresha miundombinu ya shule wilayani Tunduru. Alihamasisha ujenzi wa madarasa mapya, mabweni, na vyoo vya kisasa. Pia, alishirikiana na wadau mbalimbali wa elimu kuboresha upatikanaji wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia.
Mhe. Mtatiro ataendelea kukumbukwa kwa utashi wake wa dhati na mbinu bunifu katika kuboresha elimu pamoja na uchumi wilayani Tunduru.
Mhe. Julius S. Mtatiro akiwa katika ziara yake ya ukaguzi wa Maghala ya kuhifadhia Korosho Wilayani Tunduru.
Jumuiya ya Wilaya ya Tunduru inamtakia Mhe. Julius Mtatiro kila la kheri katika majukumu yake mapya katika Wilaya ya Shinyanga. Anaondoka Tunduru akiwa ameacha alama isiyofutika katika sekta ya elimu na usimamizi wa ajenda zote za maendeleo.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.