Mafunzo ya kina kwa watendaji wa ngazi ya jimbo ambao ni waandishi wasaidizi ngazi ya kata (ARO-Kata) kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura yamehitimishwa kwa mafanikio makubwa. Mafunzo haya yamelenga kuwajengea uwezo watendaji ili waweze kutekeleza zoezi hili muhimu kwa ufanisi na kwa kuzingatia viwango vya ubora.
Akizungumza katika hafla ya kufunga mafunzo hayo, mgeni rasmi Ndg. Chiza C Marando, ametoa wito kwa watendaji wote kuhakikisha wanashirikiana kwa karibu ili kufanikisha zoezi hili. Amesisitiza umuhimu wa kuzingatia kuwa Jimbo letu linapakana na nchi jirani, hivyo ni muhimu kuchukua tahadhari za ziada kuhakikisha kwamba wananchi wote wanaosajiliwa ni raia halali wa Tanzania.
“Ushirikiano ni muhimu sana katika zoezi hili, Nawaomba kufuata taratibu zote zilizowekwa na Tume, Pia, ni muhimu kutunza kwa makini vifaa vyote vitakavyotumika katika zoezi hili.” alisema Ndg. Marando “Tunapaswa kufanya kazi kwa pamoja ili kuhakikisha kila mwananchi anayestahili ana andikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura.”
Zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika Jimbo la tunduru kusini na kaskazini linatarajiwa kuanza tarehe 28/01/2025 hadi tarehe 03/02/2025, kila mwananchi anasisitizwa kushiriki zoezi hili kikamilifu kwani Kujiandikisha kuwa mpiga kura ni msingi wa uchaguzi bora.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.