Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji Tunduru Ndg.Abdallah H Mussa Amshukuru Rais.
Aliyasema hayo aliyekuwa Mkurugenzi Mtendeji wilaya Tunduru ndg Abdallah H Mussa wakati akiagana na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru mapema leo katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa boma.
Ndg Abdallah Mussa alianza kwa kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumuamini na kumteua kuwa Mkurugenzi Mtendaji katika Halmashauri ya wilaya ya Tunduru, na alimpongeza katika utendaji wake uliotukuka kwani katika kipindi cha miaka miwiliya uongozi wake amefanya mambo makubwa sana kwa wananchi wa Tanzania.
“katika uongozi wa rais wetu amefanikiwa kufanya mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuboresha sekta ya anga, kupiga vita rushwa na ubadhirifu wa mali za Umma, kuondoa wafanyakazi hewa katika mfumo wa Utumishi wa Umma, kuboresha huduma za afya katika hospitali na vituo vya afya, hakika namuombea mungu aendelee kumlinda katika utumishi wake kwa taifa”alisema ndg. Abdallah Mussa.
Aidha liendele kusema kuwa katika kipindi cha utendaji wake katika Halmashauri ya wilaya ya Tunduru amefanikiwa kufanya mambo makubwa katika ya sekta mbalimbali mfano sekta za Afya, Maji, Mapato, Utawala, Elimu kilimo na ushirika,pia alishirikiana wadau wa maendeleo na watumishi walikuwa chini yake katika kuwahudumia wananchi kuanzia julai 2016 hadi sasa.
Katika kipindi cha uongozi wake Mkurugenzi Mtendaji Ndg Abdallah Mussa alifanikiwa kusimamia kikamilifu katika ukusanyaji wa mapato na Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2016/2017 ilikusanya kwa asilimia 125 kutoka asimilia 80 mwaka wa fedha 2015/2016 na kuongoza katika ukusanyaji wa mapato katika mkoa wa Ruvuma.
Vilevile katika eneo la utekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia mapato ya ndani Halmashauri iliweza kutenga fedha za ndani shilingi milioni 100 katika bajeti za ujenga vyumba kumi 10 vya madarasa katika shule za msingi ili kupunguza tatizo la wanafunzi kusoma chini ya miti na mlundikano wa wanafunzi katika vyumba vya madarasa.
“niliweza kuboresha miundombinu ya shule za msingi na sekondari kwa kutenga fedha katika bajeti ya ujenzi wa madarasa, matundu ya vyoo, shule nyingi za Halmashuri ya Tunduru hazina vyoo, madarasa ni mabovu sana, na hata nyumba za kuishi watumishi ni za nyasi”alisema aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji
Sambamba na hayo Mkurugenzi Mtendaji ndg Abdallah Mussa alifanikisha kuidhinisha na kulipa fedha za mikopo ya vijana na wanawake kutoka katika makusanyo ya ndani na jumla ya shilingi milioni 100 zilitengwa na kutolewa kwa vikundi vya wanawake na vijana katika mwaka wa fedha 2016/2017.
Kaimu Afisa Utumishi wilaya Ndg John Mpangala akiandika jambo wakati watumishi wakimuaga Mkurugenzi Mtendaji Wilaya.
Aidha kufuatia ukosefu wa wodi ya wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji katika hospitali ya wilaya ya Tunduru, Halmashauri ilitenga fedha katika makusanyo yake ya ndani na jumla ya milioni 150 zilitengwa katika bajeti ya mwaka 2016/2017.
Zaidi ya shilingi million 120 kutoka makusanyo ya ndani (own Source) zilitumika kulipa malimbikizo ya madeni ya watumishi ya mishahara, likizo, uhamisho, ajira mpya hivyo kupunguza malalamiko kwa watumishi yaliyokuwa yanakwamisha utekelezaji wa majukumu yao.
Aidha alisema katika kipindi cha uongozi wake Halmashauri yake imefanya vizuri katika maonesho kilimo ya nane nane ambayo yalifanya kikanda katika kanda ya nyanda za juu kusini mkoani Mbeya, ilifanikiwa kushika nafasi ya 2 kati ya Halmashauri zote kutoka mikoa nane , na katika ngazi ya mkoa nafasi ya kwanza kati ya Halmashauri nane.
Kaimu Afisa Elimu wilaya Mwalimu Habiba Mfaume akitoa nenola shukrani kwa mkurugenzi wao wakati alipokua anakabhi ofisi kwa niaba ya watumishi wote.
“ niliweza kuwasimamia watumishi na nilipata mafanikio makubwa sana hasa katika sekta ya kilimo, Halmashauri yangu ilitoa mkulima bora kitaifa, na ilifanikiwa kushika nafasi ya kwanza katika ngazi ya mkoa, na nafasi pili kikanda kati ya mikoa 8 iliyopo katika kanda ya nyanda za juu kusini”alisema ndg Abdallah mussa
Vilevile Halmashauri ya wilaya ya Tunduru ilifanikwa kurejesha fedha za asilimia 20 za vijiji na katika mwaka wa fedha 2016/2017 jumla ya milioni 94,256,969.00 zimepelekwa kwenye vijiji kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo, ikiwa kwa miaka mingine ya nyuma fedha hizi hazikupelekwa hivyo kuleta hoja za kiukaguzi.
Hata hivyo katika kipindi cha uongozi wake Halmashauri imepata hati safi mara mbili mfululizo katika kipindi cha mwaka wa fedha 2015/2016 na 2016/2017 hivyo kuondoa hati yenye mashaka.
Kutoa mikopo kwa vikundi vya Wanawake (5%) na Vijana (5%), jumla ya shilingi milioni 197,708,760.00 zilitengwa katika bajeti yam waka wa fedha 2016/2017 kupitia makusanya ya ndani na jumla ya vikundi 10 vya vijana na vikundi 10 vya wanawake vimekopeshwa na Halmashauri.
Hata hivyo ndug Abdallah Mussa aliwataka watumishi kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano, bidii na umoja kama walivyokuwa wanafanya ili kuwatelea wananchi maendeleo ili kufikia azma ya serikali ya awamu ya tano ya kuleta maendeleo kwa wananchi kuanzia ngazi ya chini kabisa ya Kijiji.
Aliwasisitiza kuendelea kufanya kazi kwa kufuata sharia, kanuni na taratibu na kufuata misingi yote ya utumishi wa umma, kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa kuboresha huduma kwa wananchi katika Afya, Elimu, Maji, na Kilimo ili kufikia uchumi wa kati na watendaji ndio chachu ya maendeleo.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.