• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Tunduru District Council
Tunduru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
  • Utawala
    • Departiment
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu Msingi
      • Maji
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maliasili na Utalii
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Utumishi
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Information, Technology, Communication and Public Relation
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Biashara na Viwanda
    • Mining
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Kilimo
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Mifugo na Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha za Madiwani
      • Kata ya Mbati
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Time Table
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Tarajali
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa wateja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

Teknolojia ya Habari, Mawasiliano na Mahusiano


Kwa kuzingatia umuhimu wa TEHAMA na lengo la serikali la kuwa na serikali mtandao, Halmashauri ya wilaya ya Tunduru  ni miongoni mwa taasisi za serikali ambazo zinafanya vizuri katika eneo la TEHAMA.Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na uhusiano katika wilaya ya Tunduru  ni ya kuridhisha kwa sasa.

Shughuli/Majukumu ya Kitengo 

Kusimamia Mifumo yote tumizi katika Halmashauri

Kuweka na kusimamia miundo mbinu ya Mtandao Kiambo na intaneti

Kutoa msaada wa kiufundi kwa Watumiaji wa Miundo mbinu na vifaa vya TEHAMA

Kuandaa na kusimamia mifumo ya Usalama wa Kompyuta

Kusimamia utekelezaji wa shughuli kwa kutumia Serikali mtandao

Kuandaa sera ya Matumizi ya taarifa za Kompyuta

Kusimamia Mifumo yote ya TEHAMA

Kuhakikisha teknolojia ya matumizi ya mifumo ya Kompyuta inaendana na wakati na ukuaji wa Teknolojia.

Kuandaa na kufanya tafiti na kupendekeza matumizi ya TEHAMA katika shughuli ili kuboresha utoaji huduma kwa Halmashauri.

Kufanya Maboresho katika mifumo yote tumizi ya Halmashauri.

Kuandaa kituo cha utunzaji wa kumbukumbu kwa ajili ya utunzaji taarifa za mifumo

Kusimamia na Kupitia vigezo vya mifumo na utoaji huduma

Kutoa specification za vifaa kwa ajili ya manunuzi

Kushiriki katika zabuni za vifaa vya TEHAMA na kuhakiki ubora wake kabla havijaanza kutumika

Kuhakikisha Halmashauri ina tovuti na inapatikana wakati wote

Eneo la Uhusiano

Kuhakikisha tovuti ya Halmashauri ina taarifa mpya kila wakati na District profile

Kutangaza maeneo ya uwekezaji ya Halmashauri katika tovuti, radio na majarida

Kutangaza kazi na miradi inayofanyaika katika Halmashauri

Kuandaa na kutoa majarida kuhusu halmashauri

Kusimamia sera, mikakati na miongozo inayotolewa na serikali Kuu juu ya uendeshaji wa kazi za Uhusiano.

Kuandaa mpango, bajeti, mpango kazi, mpango mkakati wa kutekeleza kazi za Uhusiano katika Halmashauri

Kushiriki katika mijadala ya jamii kuhusu masuala ya Halmashauri

Kutumia Tehama katika kutoa elimu kwa jamii

Kusimamia press briefying za Halmashauri

Kushauri Halmashauri juu ya uandaaji, uzalishaji na usambazaji wa nyaraka kwa wadau mbalimbali, na

Kushirikiana kwa karibu na Afisa uhusiano wa Mkoa na wa Wizara ili kubadilishana uzoefu na kujengeana uwezo.

MAWASILIANO YA SIMU

Kampuni ya simu Tanzania (TTCL) ndiyo inayotoa huduma za mawasiliano ya njia ya simu katika ofisi zote za serikali na mashirika ya Serikali. Aidha Makampuni mengine ya simu za mkononi kama vile Vodacom,Tigo, Airtel, Halotel  yametawanyika vizuri hadi vijijini na hivyo kufanya mawasiliano kuwa rahisi zaidi. Uwepo wa Makampuni mbalimbali umewasaidia wananchi kupata taarifa mbalimbali za kijamii na kiuchumi.

VITUO VYA REDIO

Kutokana na mabadilko ya sera za habari na mawasiliano ambapo vituo binafsi vya radio vimeruhusiwa kuanzishwa, wilaya ya Tunduru  sasa ina vituo viwili (2) vya radio. Lakini bado havijaanza kurusha matangozo yake.

MATUMIZI YA MIFUMO

Hadi kufikia Februari 2017 mifumo tumizi mbalimbali ya kisekta/kiidara imefungwa katika Ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Tunduru ili kurahisisha utendaji kazi na  kuongeza ufanisi katika utoaji huduma. Mifumo hii ni pamoja na;

Mfumo wa Malipo (Epicor); Mfumo huu hutumika katika kuandaa na kutoa malipo. Mfumo huu umefungwa na utasaidia sana kupunguza hoja za ukaguzi kwa kiwango kikubwa. Mfumo huu umeunganishwa kwa kutumia mkongo wa Taifa (fibre Optics)

PlanRep (Planning and Reporting) : Huu ni mfumo unaotumika kuandaa Mpango wa Bajeti na Kutoa taarifa. Mfumo huu wa PlanRep hutumiwa na Halmashauri wakati wa kuandaa bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa.

CDR na CFR--Hii ni mifumo inayotumika kutolea taarifa za miradi ya maendeleo katika ngazi za Mamlaka ya Serikali za Mitaa.

Mfumo wa taarifa za Kiutumishi (HCMIS maarufu kama LAWSON): Huu ni mfumo unaotumika katika mishahara, kwa kutumia mfumo huu, serikali imeondoa tatizo la mishahara hewa, kuchelewa kwa stahili za watumishi n.k.

Mfumo wa Ukusanyaji Mapato (Local Government Revenue Collection Information System): Mfumo huu utumika katika shughuli za ukusanya wa Ushuru na Tozo mbalimbali za Halmashauri kwa Mujibu wa sheria.

Mfumo wa taarifa za Hospitali (Hospital Management Information System- GoT HOMIS): Mfumo huu hutumiwa na Hospitali kwa ajili ya kutunza taarifa za mbalimbali za Hospitali. Mfano, taarifa za Wagonjwa, Malipo, Dawa na Mengineyo. Kwa sasa mfumo huu umefungwa Hospitali ya Mji wa Kahama na Kituo cha Afya Mwenakulima. Maboresho yanaendelea ili uweze kufungwa katika Vituo na Zahanati zote za Halmashauri ya Mji.

HUDUMA YA INTANETI

Huduma ya intaneti Katika Halmashauri ya Tunduru hutolewa na makampuni mbalimbali. Kampuni ya simu ya TTCL ndiyo inayotoa huduma ya intaneti katika ofisi nyingi za serikali na mashirika. Aidha, makampuni ya simu za mikononi kama Vodacom, Tigo, Airtel na Zantel na halotel yanatoa huduma muhimu ya intaneti kupitia simu za mikononi na "moderm"



Matangazo

  • MATOKEO YA FORM FOUR 2022 - 2023 February 01, 2023
  • Watumishi wa Umma walioma mwezi disemba February 01, 2023
  • Orodha ya majina ya wanafunzi waliopangiwa kidato cha tano mwaka 2019 June 02, 2019
  • Taarifa ya Ziara ya Waziri Mkuu November 22, 2017
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • ZIARA YA KAMATI YA SIASA TUNDURU

    February 04, 2023
  • UPANADAJI MITI

    February 04, 2023
  • Wafugaji wasiofuata Mwongozo wa Serikali Kuondolewa Tunduru

    February 01, 2023
  • Wafugaji wasiofuata Miongozi ya Serikali Kuondolewa Tunduru

    January 31, 2023
  • Ona Zote

Video

KILO 1,147,287 ZA KOROSHO ZIMEUZWA KWENYE MNADA WA SABA TUNDURU DC
Video Nyingine

viunganishi vya Haraka

  • MATOKEO YA MITIHANI
  • Mkataba wa huduma kwa Mteja
  • muongozo wa Tehama
  • Ijue Sheria ya Umiliki wa Ardhi ya Mwaka 1999
  • Taarifa ya Ukimwi kuishia decemba 2017
  • Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Tunduru

Tovuti linganifu

  • Tovuti Kuu ya Rais - IKULU
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Idara ya Habari Maelezo

wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Tunduru

    Anuani ya Posta: 275, TUNDURU

    Simu: + 255-025-2680004

    Simu ya Nununu:

    Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz

Anuani nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Kituo

Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.