Mh. Makamu Mwenyekiti Ndg Musa Athumani Manjaule wa Chama cha ushirika cha tamcutunduru ameitangaza kampuni ya Paramount Commodities kuwa imeshinda mnada wa tarehe 15/08/2020 kununua zao la mbaazi kati ya makampuni matatu ambayo yalijitokeza ambapo kampuni ya Paramount commodities itanunua Kgs 420,756 Bei 580.00 Thamani 244,038,480.00
Pia makamu mwenyekiti amewataka wanunuzi katika mnada ujao wajitaidi kuongeza bei kwani kwa mnada huu wa kwanza bei zao ni za chini sana hivyo amewataka wajipange vizuri katika mnada ujao aidha makamu mwenyekiti huyo amesema kuwa makato kwa wanachama wake utazingatia na umbali wa wanachama wanako toka.
Aidha kabla makamu mwenyekit haja soma kampuni ambayo ilishinda mnada huo wakulima walimuomba Mh. Makamu mwenyekit wa tamcutunduru ili amnyanyue Afisa Ushirika wilaya Ndg George N.Bisani kwa lengo atoe mchanganuo wa kiasi hicho cha fedha cha bei ya Tshs 580.00 Afisa Ushirika wilaya alitoa mchanganuo huo kama alivyo agizwa na makamu mwenyekiti uku akifuata muongozo wa viwango wa vyama vya ushirika unavyo hitajika.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.